Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngorongoro yasaka ubingwa, heshima

3c70ec431114bf97a1267054cc509192 Ngorongoro yasaka ubingwa, heshima

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ leo itacheza fainali za michuano ya Cecafa dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Black Rhino, Karatu, Arusha.

Ngorongoro Heroes ilifuzu fainali hizo baada ya kuifunga Sudan Kusini kwa bao 1-0 na Uganda iliifunga Kenya 3-0.

Akizungumza jana, kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema mchezo uliopita ulikuwa mgumu lakini anashukuru kwa ushindi waliopata na kukata tiketi ya kucheza fainali za Afcon.

“Kufuzu Afcon ndio jambo jema, nawashukuru wachezaji baada ya kurudi kipindi cha pili walifanyia kazi maelekezo yangu,” alisema Julio.

Kuhusu mechi ya leo, Julio alisema kutwaa ubingwa kwa mara nyingine kwa timu hiyo ni litakuwa jambo la heshima.

“Tumefuzu Afcon ndicho tulichokuwa tunakihitaji, sasa tunataka kutwaa ubingwa ili tuweke heshima,” alisema.

Ngorongoro ambayo ilikuwa Kundi A na Djibouti na Somalia ndio timu iliyofunga mabao mengi baada ya kupachika mabao 15 na kufungwa mawili tu.

Walianza utetezi wa taji kwa ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Djibouti.

Ushindi dhidi ya Djibouti ulifuatiwa na kuisambaratisha Somalia 8-1 katika makundi.

Ni mara ya kwanza kwa Tanzania na Uganda kufuzu kwa mashindano ya U20 ya Afcon.

Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi Novemba 22 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid na Black Rhino wa Karatu yakiwa na timu 9 zilizopangwa katika makundi matatu.

Chanzo: habarileo.co.tz