Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngorongoro mabingwa,Kelvin John afunika mbaya

78649 Pic+simba

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

STRAIKA wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Kelvin John 'Mbappe' amenyakua tuzo ya Mfungaji Bora na Mchezaji Bora wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CecafaU20) 2019 jioni hii huku Tanzania ikibeba taji mbele ya Kenya.

Ngorongoro imewaduwaza majirani zao wa Kenya kwenye mechi ya fainali kwa kushinda bao 1-0, lakini furaha zaidi ikienda kwa Kelvin kwa kumaliza michuano hiyo akiwa Mfungaji Bora kwa mabao yake saba huku straika mwenzake, Andrew Simchimba akimaliza na mabao sita.

Kelvin na Simchimba washirikana na wenzao waliibeba Tanzania kwa kufunga karibu kila mechi hadi jioni hii waliposhuhudia Ngorongoro ikishinda Kombe la ubingwa wa michuano hiyo baada ya beki wa Kenya, John Otieno Onyango kujifunga dakika ya 46.

Kabla ya mechi hiyo, Kelvin alitamba ni lazima wapambane ili kubeba taji, kitu ambacho kimefanikiwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz