Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngorongoro Heroes yatema kombe

9c772ad2642192de668ba34429f24f26 Ngorongoro Heroes yatema kombe

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ imeshindwa kutetea ubingwa wake baada ya kuchapwa mabao 4-1 na Uganda katika mechi ya fainali ya michuano ya Cecafa kwenye Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha jana.

Ngorongoro Heroes licha ya kufungwa imekata tiketi ya kucheza Fainali za Afrika za U-20 (Afcon) pamoja na Uganda.

Mabao ya Uganda katika mechi ya jana ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, yalifungwa na Richard Basangwa dakika ya 12, Steven Sserwada dakika ya 40, Ivan Bogere dakika ya 61 na Kenneth Semakula dakika ya 72. La Ngorongoro Heroes lilifungwa na Abdul Suleiman kwa penalti dakika ya 30.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Sudan Kusini baada ya kuifunga Kenya kwa mabao 2-1, mabao yaliyofungwa na Philip Biajo dakika ya pili na Nelson Elia dakika ya 40 na la Kenya lilifungwa Nicholas Ochieng dakika ya 10.

Ngorongoro Heroes ilifuzu fainali baada ya kuifunga Sudan Kusini kwa bao 1-0 na Uganda iliifunga Kenya 3-0.

Ngorongoro ambayo ilikuwa Kundi A na Djibouti na Somalia ndio timu iliyofunga mabao mengi baada ya kupachika mabao 15 na kufungwa mawili tu katika makundi

Walianza utetezi wa taji kwa ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Djibouti. Ushindi dhidi ya Djibouti ulifuatiwa na kuisambaratisha Somalia 8-1 katika makundi.

Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi Novemba 22, mwaka huu katika Viwanja vya Shehe Amri Abeid na Black Rhino Karatu yakiwa na timu tisa zilizopangwa katika makundi matatu.

Kundi A ni Tanzania, Djibouti na Somalia, Kundi B lilikuwa na Burundi, Sudan Kusini na Uganda wakati katika Kundi C zilikuwa Ethiopia, Kenya na Sudan.

Chanzo: habarileo.co.tz