Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngorongoro Heroes yaichapa Sudan yatinga fainali Chalenji

78205 Pic+ngorongoro

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Timu ya taifa ya Tanzania 'Ngorongoro heroes' imefuzu kucheza fainali ya mashindano ya Chalenji kwa vijana U20 baada ya kuifunga Sudan kwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Pece War, Uganda.

Katika mchezo huo mabao ya Ngorongoro yalifungwa na mshambuliaji nyota, Kelvin John dakika 45 na Israel Patrick Mwenda dakika ya 38, huku bao la kufutia machozi kwa Sudan likifungwa na Mohhamed Abbas.

Kwa matokeo hayo Ngorongoro Heroes wanatarajia kucheza fainali dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Kenya na Eritrea.

Mshambuliaji Kelvin ameanza kuisogelea tuzo ya mfungaji bora akiwa amefunga mabao saba akimwacha nyuma Mtanzania mwingine Andrew Simchimba mwenye magoli sita.

Mchezaji huyo ambaye anahusishwa na kujiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji anakocheza mtanzania Mbwana Samatta hivi sasa amefikisha mabao saba na kuwa kinara wa ufungaji mpaka sasa kwenye mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 11 na kumuacha mwenzake Andrew Simchimba akiwa na mabao sita.

Hadi kufika hatua hiyo Ngorongoro Heroes iliyopangwa kundi B ilianza hatua ya makundi kwa kuifunga Ethiopia mabao 4-0, kisha ikatoka sare ya mabao 2-2 na Kenya halafu ikawachapa ndugu zao Zanzibar mabao 5-0 na kutinga robo fainali.

Pia Soma

Advertisement

Katika robo fainali iliichapa Uganda mabao 4-2 na kutinga nusu fainali ambayo imeifunga Sudan mabao 2-1 hivyo itacheza fainali na mshindi wa mechi kati ya  Kenya na Eritrea iliyokuwaikiendelea jana jioni.

Kocha wa Ngorongoro Heroesm Zubery Katwila ameelezea furaha yake ya kutinga fainali kwa kuwapongeza wachezaji wake kwa kupambana kila mechi na kupata matokea mazuri yaliyowawezesha kufika hatua hiyo.

"Nawapongeza wachezaji wangu kila mechi wanapambana na kufuata maelekezo yangu, mechi ya Sudan ilikuwa ngumu, lakini nashukuru tumevuka na kutinga fainali.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz