Mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Kalala Mayele ameonesha nia ya kuendelea kusalia mitaa ya Jangwani ila kinachokwamisha ni makubaliano ya mshahara na ada ya usajili ili asaini mkataba mpya utakaomuweka Yanga mpka 2026.
Fiston Mayele amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Maboss wa Yanga wanahaha kumuongezea mkataba mpya Mshambuliaji huyo aliemaliza msimu akiwa Mfungaji Bora wa NBC PL pamoja na CAFCC.
Ugumu uko wapi mpaka sasa?
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, Mayele ameweka wazi kuwa ili asaini mkataba mpya anahitaji mshahara wa Tsh Milioni 40 na Ada ya Usajili Tsh Milioni 300.
Yanga wao wamempa Ofa ya mkataba mpya wa miaka miwili utakaomfanya alipwe Tsh Milioni 35 na Ada ya Usajili Tsh Milioni 150.
Endapo Yanga watafikia dau analotaka Mayele atasaini muda wowote na kumfanya kuwa mchezaji anaelipwa zaidi huku thamani ya mkataba wake kwa miaka mitatu kuwa Bilioni 1.7 za kitanzania (Milioni 40×Miezi 36+Milioni300)
Matumaini ya Mayele kusalia Yanga ni makubwa kutokana na uhusiano wake na Maboss wa Yanga ingawa Zamalek na Pyramids wanaonekana kuanza kuteka akili ya Mcongo huyo kutokana na mzigo mkubwa waliomuandalia.