Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngolo Kante kurejea Uwanjani wiki hii

Ngolo Kante Premier League Scaled Kiungo wa Chelsea, Ngolo Kante

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa Ngolo Kante ambaye amekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu atarejea uwanjani mapema wiki hii katika mchezo wa kirafiki huku mazungumzo ya mkataba mpya yakiendelea.

Ngolo Kante amekosekana uwanjani kwa kipindi kirefu sana ndani ya timu hiyo na pengo lake likionekana mara kwa mara, Lakini mapema wiki hii mchezaji huyo atarejea dimbani na kuanza kuipambania tena klabu hiyo ya Chelsea kama iliyokua hapo awali.

Majeraha yalimfanya kiungo huyo kukosa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana 2022 na kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha kocha Didier Deschamps cha timu ya taifa ya Ufaransa, Yote ni kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimkabili kiungo huyo wa shoka.

Kante amekua akifanya mazungumzo na klabu ya Chelsea juu ya kuongezewa mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo, Huku ikielezwa mazungumzo baina yake na klabu ya Chelsea yapo kwenye hatua za mwisho hivo kiungo huyo anaweza kuongeza mkataba na kuendelea kusalia ndani ya Stamford Bridge.

Klabu ya Chelsea inaelezwa kumpa mkataba wa miaka miwili kiungo Ngolo Kante na uwezekano wa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, Hivo kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaweza kuitumikia Chelsea kwa miaka mingine miwili hapo mbele na kama ikiwapendeza klabu hiyo wanaweza kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live