Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngawina anogewa Singida FG akiwatega mabosi

Singida FG Kikosi cha Singida Big Stars

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuiokoa Singida Fountain Gate isishuke daraja, Kocha Mkuu wa muda wa timu hiyo, Ngawina Ngawina amenogewa akisema msimu wa kwanza akifundisha timu ya Ligi Kuu umempa funzo kubwa huku akiwaachia msala mabosi wa timu kuendelea kumuamini ama kumpiga chini.

Ngawina aliyeanza msimu huu kwa kuzifundisha timu za Ligi ya Championship, TMA ya Arusha na FGA Talents ya Morogoro, alikula shavu Singida Machi 7 mwaka huu akipewa mkataba wa hadi mwisho wa msimu huu akichukua nafasi ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kuiongoza katika mechi 11 akishinda tatu, sare tatu na kupoteza tano, huku akiiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya 11 ikiwa na pointi 33.

Akizungumza jijini hapa, Ngawina alisema alikuwa na kikosi finyu baada ya kufungiwa usajili na wachezaji wengi kuondoka dirisha dogo, lakini amepambana kufika hapo, huku akiamini uzoefu huo utamsaidia msimu ujao.

“Huu ni msimu wangu wa kwanza kupewa timu kama kocha mkuu naamini nitakuwa bora na kufanya vizuri. Kuhusu kama natosha kufanya vizuri na kuibeba timu hiyo ni kazi ya mashabiki, wadau na viongozi wa timu ndiyo wataona,” alisema Ngawina na kuongeza;

“Tuna kikosi kidogo cha wachezaji 20 tu, baadhi ya nafasi zina mchezaji mmoja ama hakuna lakini tumemaliza msimu vizuri, tutaorodhesha hizo changamoto na tutaziwasilisha kwa uongozi wazifanyie kazi.”

Rais wa Singida, Japhet Makau kuhusu kocha huyo alisema; “Tulimpa mkataba wa hadi mwisho wa msimu tunaomba ripoti yake atuletee, kisha tunaangalia tunajiandaaje kwa msimu ujao, pre-season tutaenda Ethiopia au Afrika Kusini.

“Tulitamani tuwe kwenye nne bora lakini ushindani ulikuwa mkubwa na sisi tukawa na changamoto kadhaa msimu haukuwa mzuri kama tulivyotegemea lakini tumemaliza nafasi ya 11, siyo mbaya ilimradi tumebaki kwenye ligi,” alisema Makau.

Chanzo: Mwanaspoti