Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngawina Ngawina aongezwa Namungo

Ngawina Mz Ngawina Ngawina

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuanza vibaya kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2024/25, Klabu ya Namungo (Wauaji wa Kusini) wameamua kuimarisha benchi la ufundi kwa kumwongeza Kocha Msaidizi, Ngawina Ngawina.

Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Klabu ya Namungo FC imethibitisha kuwa, Mkongomani Mwinyi Zahera ataendelea kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akisaidizana na Ngawina Ngawina, Shadrack Nsajigwa na Vladimir Niyonkuru.

Katika mechi mbili za mwanzo za ligi kuu ya NBC msimu huu, Namungo imepoteza mechi zote hali iliyoufanya uongozi wa klabu kufanya maboresho kwenye benchi la ufundi mapema mwanzoni tu mwa ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live