Nyota wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" na Vilabu vya Yanga, Simba na Azam FC, Mrisho Halfan Ngassa akiwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ametoa neno la busara kwa Wachezaji wa Kitanzania vijana wanaotamba katika soka kwa sasa.
Akitumia ukurasa wake wa Instagram Ngassa ameandika
"Nilipokuwa mdogo, nilipojitazama kwenye kioo, sikujiona mimi nilimuona KHALFAN NGASSA, nilimuona LUNYAMILA na nilimuona SAID MAULID ila tu nilitaka niwe zaidi yao na nafikiri hata Msuva, Sammata na vijana wengi waliofata baada yangu walipojitazama kwenye kioo waliniona MIMI ila walitaka kuwa zaidi yangu na ikawe hivyo kwako NKANE, FEISAL, HABIB KYOMBO, PASCHAL MSINDO, RABBIN SANGA, TARIQ SEIF hadi kijana mwingine anaezaliwa leo mwenye ahadi na mpira ila tu UJIONE mkubwa zaidi ili UFIKE mbali .. Huu ukawe mtindo wetu wa kuelekea kufanikiwa zaidi"
Happy Birthday to Me Happy Birthday Anko Happy Birthday Mrisho Khalfan Ngassa Ahsante?