Nyota wa zamani wa Taifa Stars, Simba, Yanga na Azam FC, Mrisho Khalfan Ngassa ametoa ushauri kwa Klabu ya Simba SCwakati huu wakijiandaa kuikabili Wydad katika mchezo wa pili wa Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.
Simba ambao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Mkapa Juma lililopita watashuka Dimbani Ijumaa ya kesho April 28 ugenini kusaka nafasi ya kutinga nusu Fainali.
Akizungumza Ngassa amewapa tahadhari Simba kwa namna walivyo bora kutumia Uwanja wao wa nyumbani.
“Simba wanaenda kukutana na timu ambayo inajua kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani, ila naamini kama watakuwa makini na mbinu zao watashinda,” amesema Ngassa