Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngassa ataja siri yake na Kikwete safari ile ya Marekani

Ngasaa Pic Data Ngassa ataja siri yake na Kikwete safari ile ya Marekani

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

WINGA machachari wa Gwambina FC, Mrisho Ngassa amefichua siri kwamba mtu aliyefanikisha safari yake ya kwenda kucheza mchezo wa kirafiki uliowakutanisha Seattle Sounders ya Ligi Kuu ya Marekani dhidi ya Manchester United ya England, ni Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete.

Ngassa alienda nchini Marekani mwaka 2011 wakati akiwa anaichezea Azam FC, alikaa katika klabu ya Seattle Sounders kwa wiki mbili na kucheza mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Man United Julai 20 mwaka huo.

Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti yaliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Ngassa alisema watu wengi wanadhani alienda Marekani kufanya majaribio lakini haikuwa hivyo kwani ulikuwa ni mualiko kutokana na ukaribu wa Marekani na Tanzania kwa kipindi hicho.

“Unajua kipindi kile cha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni wajina wangu, kulikuwa na ukaribu sana na Marekani, kwahiyo alipohitajika mtu wa kupewa nafasi ya kwenda kwenye ile mechi basi nilichaguliwa mimi, nakumbuka nilikuwa na Zamunda (Rahim Kangezi, mmiliki wa klabu ya African Lyon),” alisema Ngassa.

Alisema alipofika nchini humo alifanya mazoezi pamoja na wachezaji wa timu hiyo ya Ligi Kuu ya MLS kwa wiki mbili na ilipofika wakati wa mechi alipewa nafasi akianzia benchi.

“Niliingia nikitokea benchi, baada ya mchezo kumalizika walinishukuru na kunitakia kila la kheri nirudi Tanzania, lakini haikuwa majaribio, ila sasa watu wengi walikuwa wanaongea huku wakiwa hawajui ukweli wowote,” alisema.

Related Mkenya agundua mazito Yanga Namungo yaamua jambo kwa Simba, Yanga Simba Do or DieNgassa alifunguka zaidi na kusema licha ya kwamba alikuwa ameenda kwa ajili ya mechi hiyo, hakutoka patupu kwani alipata takribani Dola za Kimarekani 100 (Sh 200,000) kwa siku kwa wiki mbili.

Katika mechi hiyo, chama la Ngassa lilipasuka mabao 7-0 huku kikosi cha Man United kilihusisha mastaa wakubwa kama Wayne Rooney, Patrice Evra, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Jonny Evans, Luis Nani, Ryan Giggs, Ji-Sung Park, Michael Owen, Ashley Young na Michael Carrick.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz