Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngassa ashindwa kuisaidia Gwambina

B67dae5bd21d9771b6fcbfae67a90ad5 Ngassa ashindwa kuisaidia Gwambina

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSHAMBULIAJI Mkongwe kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Mrisho Ngassa ameshindwa kuisaidia timu yake mpya ya Gwambina FC, baada ya jana wakiwa uwanja wa nyumbani wa Gwambina Complex kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Biashara ya Musoma.

Ngassa aliyepata kutamba na klabu mbalimbali ikiwemo Yanga, Simba na Azam FC amejiunga na Gwambina kwenye dirisha dogo la usajili, lakini alishindwa kuisaidia timu hiyo kuepuka na kipigo na kufanya timu hiyo kupoteza mchezo wa pili msimu huu kwenye uwanja wa nyumbani.

Bao pekee la Biashara United katika mchezo huo lilifungwa na Deogratius Judika dakika ya 15 ya mchezo hiyo ilitokana na uzembe uliofanywa na mabeki wa Gwambina kushindwa kuuondosha mpira kwenye eneo l a hatari.

Gwambina ambao pia walimtumia mshambuliaji Salum Ayee walimsajili kwenye dirisha dogo kutoka KMC walijaribu kupambana kwa kushirikiana na nahodha Paul Nonga, lakini hadi mapumziko matokeo yalibaki bao 1 kwa wageni Biashara na wenyeji 0.

Kipindi cha pili kocha wa Gwambina Novatus Fulgence alimtoa Ayee na kumuingiza Rajabu Rashidi mabadiliko yaliyoonekana kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na dakika ya 58 Vedastus Mayuga alipoteza nafasi ya wazi akiwa amebaki na kipa wa Biashara Deo Mgore.

Mara walizoa pointi zote tatu na kujikita nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 29.

Chanzo: habarileo.co.tz