Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngassa: Hii Yanga ni tishio kuliko zote zilizopita

Ngassa Mzize 0768 Ngassa: Hii Yanga ni tishio kuliko zote zilizopita

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kuwa kikosi cha Yanga cha msimu huu ni tishio kuliko Yanga yoyote ambayo amewahi kuishuhudia maishani mwake.

Ngassa ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amemwagia maua yake kinda wa Yanga, Clement Mzize ambaye amekuwa akionesha uwezo bora anapopata nafasi.

Mzize amekuwa chaguo la pili kama si la kwanza kwa Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi na jana aliifungia timu yake bao la pili ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa 16 bora wa Kombe la Shirikisho la CRDB Bank huku akiwa kinara wa mabao kwenye ligi hiyo mpaka sasa akiwa na mabao 5.

"Yanga hii ni Bora toka niijue. katika miaka hii miwili Toka naijuwa Yanga Mashabiki Wana Enjoy Sana, wanaenda uwanjani wakijuwa watashinda"

"Niwape ushauri Mashabiki wa Yanga, wampe saport Mzize ni mtu hatari sana kushinda wote wanaowapenda au ambao waliwahi kuwapenda," amesema Mrisho Ngassa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live