Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NgaoYaJamii: Simba Queens vs JKT Queens ni fainali ya kibabe

Simba Queens Vs JKT Queens #NgaoYaJamii: Simba Queens vs JKT Queens ni fainali ya kibabe

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiyemtaka kaja. Ndio ukweli ulivyo kwenye fainali ya Ngao ya Jamii kwa ajili ya uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL).

Simba Queens na JKT Queens zinakutana uso kwa uso baada ya kila moja kupenya kwenye mechi za nusu fainali za michuano hiyo mipya iliyoanzishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zikihusisha timu zilizoshika nafasi nne za juu kwa msimu uliopita.

Michuano hiyo imekuja na mfumo wa timu nne kama ulivyotumika kwa mara ya kwanza kwenye uzinduzi wa Ligi Kuu Bara na Simba kubeba taji mbele ya Yanga.

Simba Queens imepenya hadi fainali baada ya kuifyatua Yanga Princess kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya timu hizo kushindwa kufungana kwenye muda wa kawaida katika pambano kali na tamu lililopigwa Uwanja wa Azam Complex, mara baada ya JKT Queens kuisambaratisha Fountain Gate Princess kwa mabao 5-0.

Timu hizo zinazokutana kwenye fainali itakayopigwa kesho Jumanne zinataka kuweka heshima na rekodi ya kuwa klabu za kwanza kubeba taji hilo, lakini kuendelea ubabe baina yao, kwani zina upinzani mkali kwelikweli kwenye WPL, kwa kupokana mataji kwa misimu sita tofauti iliyopita.

Kama hujui JKT Queens ilibeba taji la WPL kwa misimu miwili mfululizo kabla ya Simba kuipoka na kukaa na kombe hilo kwa misimu mitatu mfululizo na msimu uliopita, Maafande wa JKT wakafanya kweli kwa kulirejesha taji hilo mikononi, hivyo kufanya fainali ya kesho kuwa ni zaidi ya mechi.

MSHINDI WA TATU Ni kama ratiba ilivyo ndivyo ilivyo kwenye michuano hii, fainali inazikutanisha timu zilizomaliza kwenye nafasi mbili za juu katika Ligi Kuu ya msimu uliopita, yaani JKT iliyobeba taji na Simba iliyotemeshwa ubingwa lakini ikamaliza kwenye nafasi ya pili ya msimamo.

Kabla ya mechi hiyo ya kusaka bingwa mpya na wa kwanza wa michuano hiyo, mapema litapigwa pambano la kusaka mshindi wa tatu, linalozikutanisha pia timu zilizomaliza kwenye nafasi ya tatu na nne ya msimamo wa WPL, yaani Fountain Gate Princess dhidi ya Yanga Princess zilizochemsha juzi mbele ya Simba na JKT.

Hii sio mechi ya kubeza kutokna na upinzani mkali uliokuwepo baina ya timu hizo kila zinapokutana kwenye mechi tofauti zikiwemo za WPL, huku turufu ikiwabeba zaidi Fountain mbele ya Yanga Princess.

Utamu zaidi ni kwamba timu zote zina vikosi imara na zinajuana vizuri na mara nyingi zinapokutana kwenye ligi haijawahi kuwa mechi nyepesi hata kidogo.

UTEJA WAFUTWA Kwa miaka ya hivi karibuni Yanga inaanza taratibu ya kufuta uteja mbele ya watani wao wa kufungwa mabao mengi kwani mara ya mwisho timu hizo kukutana zilitoka sare ya bao 1-1 kila moja nyumbani kwake.

Hii inaonyesha ni kiasi gani Yanga inaanza kukua na kuthibitisha  ukubwa  wake na kama msimu huu itaendelea ilipoishia basi tutaona soka la ushindani.

Licha ya kuonesha ushindani huo lakini bado kikosi hicho kinaonekana kuwa na mabadiliko ya kiuchezaji chini ya Mzambia, Haalubono Charles aliyechukua mikoba ya Sebastian Nkoma.

VITA YA MAKOCHA WAZAWA Vikosi vyote viwili vinaongozwa na makocha wazawa, Simba ikiwa na Juma Mgunda na msaidizi wake Mussa Mgosi huku JKT ikiwa na mwanamama, Esta Chabruma.

Wote hawa wanalifahamu soka la Tanzania japokuwa kwa Mgunda ipo tofauti kutokana alizoea kufundisha wanaume na amekaa na kikosi cha wanwake si chini ya wiki mbili huku Chabruma akiwajua vyema wachezaji wake kwa kukaa nao tangu wanabeba ubingwa wa CECAFA.

Hivyo, fainali hiyo ina vita nyingi hasa na kwenye mchezo huo sasa mbinu ya kocha mmoja itaamua nani abebe ubingwa huo.

Sio tu kwenye Ngao ya Jamii mpaka kwenye ligi kwani timu tatu za juu zinaongozwa na makocha wazawa pamoja na Fountain ikiwa chini ya Masoud Juma huku Yanga ikiwa chini ya hayati Mzambia Haalubono.

DERBY YENYEWE Ilikuwa ni mchezo mzuri wa kuutazama na ukiangalia aina ya mchezaji mmoja mmoja utagundua ubora wao kwani kila mmoja alionyesha kiwango bora.

Kwa Simba kuna wachezaji kama Violeth Nickolas, Ruth Nkosi, Mwanahamisi Omary na Vivian Corazone ambao walionesha uzoefu mkubwa kwenye mechi hiyo na kuibeba kwa asilimia kubwa.

Wengine kina Elizabeth Wambui ambaye amesajiliwa msimu huu ni vile mechi ya kwanza lakini winga huyo aliisumbua Yanga kwa nguvu aliyonayo na spidi yake lakini alikosa namna nzuri ya kumalizia.

Kwa Yanga kuna Saiki Atinuke ambaye licha ya wenzake kufanya makosa lakini aliziba alisawazisha makosa hayo, anakaba vizuri na akili nyingi ya kuituliza timu.

Precious Christopher kiungo mshambuliaji aliyejitoa kwa uwezo wake binafsi na kupiga pasi ambazo zilifika kwa washambuliaji ila umakini wa kumalizia tu ilikuwa shida kwao na kwa waliomtazama juzi waliona ubora wake.

WASIKIE MAKOCHA Kocha wa Simba, Mussa Mgosi alisema wanaenda kufanyia kazi makosa waliyoyaona kwenye mechi ya nusu fainali wanaenda kukutana na JKT ambayo ilikuwa bora sana.

“Yanga walitusapraizi hatukujua kama watacheza vile wameonesha ushindani wa hali ya juu, naamini makosa tuliyoyafanya tutayafanyia kazi, JKT tuliwaona wakicheza na Fountain sio timu ndogo,” alisema Mgosi.

Kocha wa Yanga Princess, Haalubono Charles aliwapongeza Simba kwa kuonyesha upinzani aliahidi kuyafanyia kazi makosa yao.

“Kuna makosa hasa eneo la ushambuliaji halikuwa bora sana, tunaenda kwenye mechi nyingine ya mshindi wa tatu naamini tutafanyia kazi hilo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live