Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngao ya Jamii sio Kombe - Saleh Jembe

Yanga NGAO BINGWA Ngao ya Jamii sio Kombe - Saleh Jembe

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally 'Jembe' amesema kuwa, Ngao ya Jamii sio kombe kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai.

Jembe amesema hayo kufuatia Yanga kushinda taji hilo na kusema kuwa wameshinda 'treble' yaani makombe matatu ikiwa ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la SHirikisho msimu uliopita.

"Haiwezekani Ngao ya jamii mkawa mnahesabu kama kombe, hakuna makombe matatu, nimeanza kuisema hii tangu Simba wakichukua mfululizo.

"Uliwahi kuona wapi Kombe la mechi moja? Hiyo ni Super League pekee ambayo anakutana bingwa wa Champions League na Europa Cup.

"Lakini mechi inakutanisha Bingwa na mshindi wa pili hiyo ni mechi ya Ngao ya Hisani a unaihesabu tu kama Ngao, ile hauhesabu kamataji. Hata msimu huu licha ya timu nne ila ni Ngao tu.

"Mataji ni yale yanafayofanya timu zetu zikacheze michuano mikubwa ya Afrika, labda irudishwe Kombe la Muungano," amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live