Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngao ya Jamii iwe chachu maandalizi ya Kitaifa na Kimataifa

Simba Queens Ngao Ya Jamii 2023.jpeg Ngao ya Jamii iwe chachu maandalizi ya Kitaifa na Kimataifa

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tumeshuhudia namna maendeleo kwenye sekta ya soka la Wanawake Tanzania namna yanavyopiga hatua kila iitwapo leo.

Kwa wakati huu ni Simba Queens walitangazwa kuwa mabingwa wa Ngao ya Jamii Wanawake kwenye fainali iliyohusisha timu nne pale Uwanja wa Azam Complex.

JKT Queens wanakuwa washindi wa pili huku Yanga Princess wao wakiwa ni washindi wa tatu na Singida Fountain Gate nafasi ya nne.

Kwa muda mfupi ambao mashindano yalikuwa yanaendelea tumeshuhudia namna wachezaji walivyokuwa na kiu ya kufanya kweli katika kila mechi kwa kuchukulia kila mchezo ni fainali.

Maandalizi yake pia hayakuwa yakubeza kwa kuwa muitikio ulikuwa mkubwa. Mashabiki na kila mmoja ambaye alijitokeza anastahili pongezi kwa kuwa sehemu ya historia kwenye maendeleo ya soka la Wanawake.

Bado kila timu ilipata nafasi ya kuona mapungufu yake hivyo ni muhimu kufanyia maboresho kwa ajili ya wakati ujao kupata kilicho bora.

Kukamilishwa kwa Ngao ya Jamii hii inamaana kwamba Ligi ya Wanawake inakwenda kuanza hivyo maandalizi yanapaswa kuwepo kwenye kila idara.

Hakuna timu ambayo ni yakubeza kwa sasa kutokana na maandalizi ambayo yapo na picha inaonesha kwamba ushindani utakuwa mkubwa kila kona.

Kushinda kwa Ngao ya Jamii Wanawake sio mwisho wa mapambano ni lazima kazi iendelee na wale ambao hawajashinda haina maana kwamba hawana uwezo bali ni muhimu kujipanga kwa wakati ujao na inawezekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live