Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ng'ombe wa Mayele ashushwa Jangwani, GSM apewa Mbuzi (+Video)

Video Archive
Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Februari 23 mwaka huu, Yanga ilikuwa Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Manungu ikikipiga na Mtibwa Sugar katika mchezo ulioteka hisia za wengi kutokana na rekodi nzuri ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wake wa nyumbani.

Baada ya dakika 90 za mtanange huo kukamilika, Yanga waliibuka na ushindi wa magoli 2-0 yaliyowekwa kimiani na Saido Ntibazonkiza mwishoni mwa kipindi cha kwanza na Fiston Mayele kipindi cha Pili.

Goli lililofungwa na Mayele lilimuamsha Shabiki wa Wanajangwani aliefahamika kwa jina la Mauya na kutoa ahadi ya kumpa Straika huyo Mkongo Zawadi ya Ng'ombe mbele ya Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli na Kocha Nabi.

Sasa Shabiki huyo amekamilisha ahadi yake baada ya kufika Makao Makuu ya Yanga mtaa wa Jangwani na kumkabidhi ngombe huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live