Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar kuwakosa Cameroon

Neymar Kukosa Mechi Mbili Zijazo Akiuguza Jeraha La Mguu Neymar

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr kukosekana kwenye mchezo wa mwisho wa kufunga hatua ya makundi dhidi ya timu ya taifa ya Cameroon.

Mchezaji huyo ambaye alipata majeraha katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Serbia baada ya kuumizwa enka na kumfana kukosa mchezo wa pili wa kundi dhidi ya Uswisi huku ilizaniwa kama atakuepo kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Cameroon lakini imeshindikana.

Neymar anatarajiwa kurudi kwenye hatua ya 16 bora ambapo timu yake tayari imefuzu baada ya kuifunga timu ya taifa ya Uswisi hapo juzi.

Ukiachana na staa huyo timu ya taifa ya Brazil pia imeongeza majeruhi kwani katika mchezo wa kwanza aliumia Neymar pamoja na Danilo. Lakini taarifa iliyotoka ni kua beki wa kushoto Alex Sandro nae ataukosa mchezo wa mwisho dhidi ya Cameroon akiuguza maumivu ya nyonga.

Mpaka sasa timu ya taifa ya Brazil itawakosa mabeki wake wa pembeni katika mchezo wa mwisho dhidi ya Cameroon na itamlazimu mwalimu kuwatumia wachezaji chaguo la pili kwenye nafasi hizo ambapo itakua haina athari sana kwakua timu hiyo tayari imefuzu hatua inayofuata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live