Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar kukosa mechi mbili zijazo akiuguza jeraha la mguu

Neymar Kukosa Mechi Mbili Zijazo Akiuguza Jeraha La Mguu Neymar kukosa mechi mbili zijazo akiuguza jeraha la mguu

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Neymar hatashiriki mechi mbili zijazo za Brazil za Kombe la Dunia baada ya kupata jeraha la mguu wa kulia, anasema daktari wa timu yao.

Mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 aliondolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo wa siku ya Alhamisi ambapo Brazil waliichapa Serbia 2-0 baada ya kukabiliwa vikali na Nikola Milenkovic.

Neymar aliketi huku uso wake ukiwa umefunikwa wakati alipokuwa akipata matibabu na picha zilionyesha fundo lake la mguu wa kulia likiwa limevimba.

Chanzo: Bbc