Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar kapata shemeji mwingine

Neymar Jr Shemeji Neymar kapata shemeji mwingine

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Dada wa supastaa, Neymar, Rafaella Santos amehakikisha kwamba hajiweki mbali na watu wa mpira baada ya kuangukia tena kwenye penzi la mwanasoka.

Mrembo Rafaella, ambaye amemfanya kaka yake kughushi sana majeraha na wakati mwingine kujipatisha kadi za makusudi kila inapofika siku ya kuzaliwa ya dada huyo ili akahudhurie, kwa sasa yupo kwenye penzi la moto na mwanasoka Joaquin Piquerez.

Piquerez kwa sasa anaichezea klabu ya Palmeiras ya Brazil kwenye nafasi ya beki wa kushoto, huku akiwa anaitumikia Uruguay kwenye soka la kimataifa, ambapo hadi sasa amecheza mechi 13 akianzia mwaka 2021.

Beki huyo aliibua uvumi wa kuwa na uhusiano na Rafaella baada ya kuhudhuria sherehe za siku za kuzaliwa za mrembo huyo alipotimiza umri wa miaka 28, ambapo aliandamana na wachezaji wenzake wa Palmeriras.

Rafaella huko nyuma aliwahi kuwa na uhusiano na mwanasoka, straika Gabriel Barbosa (aliyekumbatiana naye pichani).

Barbosa, anayefahamika kama ‘Gabigol’, alianza kudeti na dada huyo wa Neymar mwaka 2017, lakini wawili hao sasa wameachana na Rafaella, mwenye wafuasi milioni sita huko Instagram yuko na mpenzi mpya.

Rafaella anafanya shughuli za mitindo na alijiweka kuwa maarufu zaidi alipotokea kwenye tangazo la Kombe la Dunia la Beats la Dre mwaka 2014.

Rafaella amekuwa kipenzi kikubwa cha Neymar, ambaye kwa sasa ni mchezaji wa klabu ya Al-Hilal aliyojiunga nayo akitokea PSG wakati wa dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Na kinachoelezwa ni kwamba Neymar anasapoti uhusiano huu mpya wa dada yake na mwanasoka Piquerez, kuliko wakati ule alipokuwa akitoka na Mbrazili mwenzake, Barbosa.

Chanzo: Mwanaspoti