Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar atoa kauli ubora wa Casemiro

Casemiro Appraised Kiungo wa Brazil, Casemiro

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amemsifu Casemiro kama “kiungo bora zaidi duniani” baada ya mchezaji huyo kuwapeleka Brazil katika hatua 16 bora ya Kombe la Dunia dhidi ya Uswizi hapo juzi huku bao hilo likifungwa dakika za jioni kabisa.

Baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu katika mechi ya ufunguzi ya Kundi G ya Selecao, mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain alilazimika kutazama mechi ya pili ya timu yake kutoka hotelini kwao.

Katika mechi hiyo kali, bao la dakika za mwisho la kiungo wa kati wa Manchester United ndilo liliipatia Brazil ushindi wa 1-0, na Neymar hakusita kutoa sifa zake kwa ufupi kumsifu mchezaji mwenzake baada ya filimbi ya mwisho akiandika katika Twitter kuwa;

“Casemiro amekuwa kiungo bora zaidi Duniani kwa muda mrefu,”

Alipoulizwa na Stats Perform katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi kama alikubaliana na Neymar, Tite alijibu: “Kama kawaida, mimi huheshimu maoni, lakini sitoi maoni juu yao, lakini nitajiruhusu kufanya hivyo leo. Nakubali.”

Akielezea kwa nini alichagua kumchezesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 katika nafasi ya kina zaidi, aliongeza:

“Casemiro ni kiungo wa pili, ndivyo tulivyoona vikitokea anafanya kazi kama mchezaji wa kati, ni kitu cha kushangaza kutoka nyuma. Ikiwa Casemiro tayari yuko juu, ni rahisi kutambuliwa, lakini anapotoka nyuma anaweza kushtukiza.”

Brazil watamaliza kampeni yao ya Kundi G dhidi ya Cameroon mnamo Desemba 2 huku wakiwa wameshikilia hatma ya timu hiyo kutoka Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live