Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar arudi mazoezini PSG

Neymar And Kylian Mbappe Xbwlnmwkxt5l1fbl4wtiy0ehn Neymar arudi mazoezini PSG

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Neymar anaweza kuwa sehemu ya mchezo wa Paris Saint-Germain dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Februari 15.

Nyota huyo wa Brazil amekuwa nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu tangu Novemba lakini alirejea mazoezini Alhamisi siku tano tu kabla ya mtanange wa kwanza kati ya wababe wawili wa Ulaya huko Parc des Princes.

Neymar ambaye alitimiza umri wa miaka 30 wikendi iliyopita alitumia zaidi ya wiki sita na alikosa mechi 12 za timu hiyo yenye maskani yake mji mkuu wa Ufaransa Paris.

Sergio Ramos anabakia kuwa na shaka na tatizo lake la mguu kuelekea mchezo dhidi ya klabu yake ya zamani.

“Ni mchezaji mkubwa ambaye anapaenda kucheza dhidi ya timu kubwa,” Pochettino alisema wakati wa mkutano na waandishi kabla ya mechi dhidi ya Rennes “Lakini pia ni mchezaji ambaye amepitia hali ya majeraha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live