Kocha wa Al Hilal, Jorge Jesus amefichua siri kwamba Neymar ana majeraha na hatakuwa fiti kucheza mechi ya kimataifa akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Brazili mwezi ujao.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Jesus ambaye ndio kwanza ameanza kibarua baada ya kuteuliwa amethibitisha kuwa Neymar ni majeruhi na ameshangazwa amejumuishwa katika kikosi cha Brazili kitakachocheza dhidi ya Peru na Bolivia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa nje ya dimba kuanzia Februari mwaka huu kufuatia upasuaji wa kifundo cha mguu.
“Neymar amejiunga na Al-Hilal akiwa na majeruhi, ana matatizo kidogo, hatufahamu atarejea dimbani lini, sidhani kama anastahili kuwepo katika kikosi cha Brazili na hatakiwi kusafiri umbali mrefu,” alisema kocha huyo.