Staa wa PSG, Neymar Jumanne ya wiki hii alipoteza pauni 900,000 baada ya kuliwa kwenye kamari ya mtandaoni.
Nyota huyo wa Paris Saint- Germain na Brazil kwa sasa yuko nje ya dimba akiuguza enka aliyoumia hivi karibuni na atakuwa nje kwa msimu huu wote uliobaki.
Juhudi za Neymar kushinda kamari hiyo mbele ya watu wengi zilishindikana na kujikuta akiliwa.
Mbrazil huyo alicheza kamari hiyo kwenye Casino ya mtandaoni huko Las Vegas kwa kutumia dakika 60 na kujikuta akipoteza fedha hizo nyingi na kusababisha apatwe na huzuni.
Katika video fupi iliyopostiwa mtandaoni ilimuonyesha Neymar akiangua kilio kwa sauti kubwa kabla ya kubadilika haraka na kuanza kucheka.
Hata hivyo kiasi hicho cha pesa alichopoteza ni kama tone tu la maji kwa Neymar ambaye inasemekana anakunja pauni milioni 3.4 kwa mwezi pale PSG.
Baada ya Neymar kuliwa, shabiki mmoja alisikika akisema: "Ninamuhurumia, lakini Aprili anakuja na anarudishiwa pesa zake."