Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar aomba radhi kwa mpenzi wake hadharani

Neymar Msamaha Neymar

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Supastaa wa Kibrazili, Neymar ameweka kando ugumu wote na kuomba radhi hadharani akimtaka mpenzi wake ambaye ni mjamzito, mrembo Bruna Biancardi amsamehe huku akisisitiza: “Nimefanya makosa.”

Staa huyo wa PSG, Neymar, 31, na Biancardi, 29, walithibitisha Aprili mwaka huu kwamba wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

Hata hivyo, taarifa hizo ambazo Neymar alizitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram alipoweka picha yake na ya mpenzi wake, inaonekana kumtibua mrembo Bruna, kwa sababu hakutaka mambo ya ujauzito wake ujulikane hadharani na jambo linalomfanya Neymar kuomba radhi ili asimpoteze mrembo wa maisha yake.

Staa huyo wa zamani wa Barcelona alisema: “Bru, nafanya hivyo kwa ajili yako na familia yako. Hebu jaribu kufikiria. Hakuna haja ya kuendeleza matatizo, tunakuhitaji sana kwenye maisha yetu.

“Nimeona namna gani nilivyokuanika, najua ni jinsi gani hukupendezwa na hilo, lakini naona wazi jinsi ninavyokuhitaji uwe karibu yangu. Nipo pamoja nawe. Nimefanya makosa. Nimekosea sana.

“Nathubutu kusema nimekuwa nikikosea kila siku, ndani na nje ya uwanja. Lakini, makosa yangu binafsi ninayofanya nyumbani, namalizana nayo kwa ubinafsi huohuo na familia yangu na marafiki “Lakini, hii imemhusu mtu spesho sana katika maisha yangu. Mwanamke ambaye nimekuwa na ndoto za kuwa naye karibu, mama wa mtoto wangu. Niliikosea familia yako, ambayo ni familia yangu pia. Niliingilia mambo yako binafsi katika kipindi hiki ambacho ungehitaji usiri mkubwa.”

Neymar aliendelea: “Bru, nimeshaomba radhi kwa makosa yangu, kwa kukutangaza bila ya sababu ya msingi, lakini najiona nalazimika kulieleza hili hadharani. Kama vitu binafsi viliwekwa hadharani, basi hata msamaha uombwe hadharani. Sipati picha maisha bila ya wewe. Nakupenda.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live