Wed, 27 Sep 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mshambuliaji wa Brazil, Neymar Jr amekosoa ripoti zilizosambazwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba ameitaka klabu yake ya Al Hilal ya Saudi Arabia kumfuta kazi kocha Jorge Jesus na kusisitiza kuwa ripoti hizo ni uzushi.
Kocha huyo raia wa Brazil aliripotiwa kumkosoa Neymar kwa tabia yake uwanjani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Asia kati ya Al Hilal dhidi ya Navbahor Namangan hali iliyopelekea kutoelewana kwa wawili hao.
Baadaye iliripotiwa kuwa Mbrazil huyo ameitaka klabu hiyo kumfukuza kocha huyo lakini sasa Neymar amekanusha ripoti hizo na kudai ni uongo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live