Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar afutiwa mashitaka ya ulaghai

Neymar Jml.jpeg Neymar afutiwa mashitaka ya ulaghai

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka yaliyohusu usajili wake mwaka 2013 kutoka Santos kuhamia Barcelona amefutiwa mashitaka hayo.

Neymar alidaiwa kuwa usajili wake huo ulikiuka baadhi ya masuala ya kifedha na kukwepa kulipa kiasi kadhaa cha fedha wakati wa uhamisho wake huo.

Katika kesi hiyo waendesha mashtaka walitaka nyota huyo ahukumiwe miaka miwili jela na faini ya Paundi Milioni 8.6m (Tsh Bilioni 23.1), lakini wameamua kufuta mashitaka yao yote dhidi ya Neymar na wengine waliyokuwa wakihusika na kesi hiyo.

Wengine waliyokuwa wakishtakiwa ni wazazi wa Neymar, Marais wa klabu zilizohusika katika usajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live