Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar afanyiwa upasuaji Qatar

Neymar Upasuaji Neymar afanyiwa upasuaji

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Paris Saint-Germain, Neymar amefanyiwa upasuaji wa enka jambo linalomfanya kuwa nje ya uwanja msimu mzima.

Fowadi huyo Mbrazili amekuwa nje ya uwanja tangu Februari alipomia kwenye mechi ya Ligue 1 dhidi ya Lille, ambapo alitolewa uwanjani huko machozi yakiwa yanambubujika.

Na sasa mkali huyo wa kimataifa wa Brazil, alifanyiwa upasuaji huko Aspetar, hospitali rasmi washirika wa PSG iliyopo Doha, Qatar. Upasuaji huo ulifanikiwa na mchezaji huyo alionekana akionyesha ishara ya dole gumba wakati alipokuwa akipigwa picha.

Neymar anatarajia kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu na upasuaji huo ilifanikiwa ili kumwondoa Neymar kwenye madhara ya kuumia zidi. Upasuaji huo ulisimamiwa na profesa Peter D’hooghe, ukifanyika na speshalisti wa enka Pierre James Calder na daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar.

Kuumia kwa Neymar kumewafanya Lionel Messi na Kylian Mbappe kupaki wenyewe kwenye fowadi ya PSG na sasa timu hiyo inatumia fomesheni ya 3-5-2. Pengo lake lilikuwa kubwa na hivyo PSG kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya 16 bora mbele ya Bayern Munich baada ya kuchapwa 2-0 wiki iliyopita huko uwanjani Allianz Arena, hivyo kuondoshwa kwenye michuano hiyo kwa msimu huu kwa jumla ya mabao 3-0.

Neymar amekuwa akisumbuliwa na majeruhi makubwa mara kadhaa tangu uhamisho wake wa pesa nyingi wa Pauni 198 milioni alipotoka Barcelona kwenda kujiunga na PSG mwaka 2017. Ndani ya muda huo, Neymar amekosa zaidi ya mechi 100.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live