Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar Jr hali tete tena

Neymar Kilio Ds Neymar Jr hali tete tena

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr amepata majeraha ya goti wakati akiitumikia #Brazil alipokuwa akiwania mpira na Nicolas de la Cruz katika dakika ya 44 ya mchezo ambao timu yake ilipoteza kwa magoli 2-0 dhidi ya Uruguay.

Al-Hilal imetoa taarifa kuwa atafanyiwa upasuaji lakini haijaweka wazi muda atakaoutumia kuwa nje ya Uwanja.

Kwa aina ya jeraha alilopata kuna uwezekano pia akaikosa Michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza Juni 2024 Nchini Marekani.

Amepata changamoto hiyo ikiwa ni miezi miwili tangu Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imsajili, ambapo alisaini Mkataba wa kulipwa Pauni Milioni 130 (Tsh. Bilioni 395) kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live