Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar Jr amtaja mshindi wa Ballon d'Or

Neymar Al Hial Sm Neymar Jr

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Al Hilal ya Saudi Arabia, Neymar Jr ameweka wazi kumuunga mkono mbrazili mwenzake Vinicius Junior anayekipiga Real Madrid kwamba ndiye atakayeshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka huu.

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amefurahia msimu mwingine mzuri zaidi, akishinda mataji ya UEFA na La Liga. Hata alijinyakulia bao katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Los Blancos walipoizamisha Borussia Dortmund.

Hilo limemfanya Neymar kudai mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hakika atatawazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2024.

Kwa sababu hiyo Neymar anaamini kuwa Vinicius Junior amekuwa mchezaji bora wa dunia mwaka 2024 hivyo anastahili kushinda Ballon d'Or.

Neymar anaamini Vini ataiongoza vyema nchi yake ya Brazili katika michuano ya Copa America msimu huu wa joto na kutwaa ubingwa wa kombe hilo.

Vinicius alifunga mabao sita kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, na hivyo akatajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo kwa msimu wa Mwaka 2023/24.

Pia, alichaguliwa katika timu bora ya La Liga baada ya kuisaidia Real Madrid kutwaa taji lingine la Uhispania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live