Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neymar Arsenal?

Mm Neymar Neymar Arsenal

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa za zamani wa Arsenal na Brazil, Gilberto Silva anaamini inawezekana kabisa Neymar kutua kwa washika mitutu katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Neymar ambaye alijiunga na Al Hilal dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana akitokea PSG, hajawa na nyakati nzuri nchini humo kutokana na majeraha aliyoyapata muda mfupi tu baada ya kuanza kucheza.

Licha ya timu yake kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Saudi Arabia msimu uliopita, Neymar alichangia kwa kucheza mechi tatu tu na kutoa asisti tatu.

Huu ulikuwa ni mwaka wa kwanza kwa Neymar kucheza nje ya Ulaya tangu alipotua barani humo mwaka 2013 kujiunga na Barcelona.

Kutokana na kinachomtokea sasa akiwa na Al Hilal, Gilberto anaamini anaweza kufikiria kurudi Ulaya na ikiwa hivyo kutua Arsenal inawezekana.

“Ningependa kumWona Neymar Ligi Kuu England akiichezea Arsenal, itakuwa ni kitu cha kuvutia, naamini mashabiki watafurahi na hata ligi pia itakuwa tamu zaidi. Nafikiri mtu anapotazama ligi hii anatakiwa kuona wachezaji bora zaidi duniani, hivyo Neymar akitua hilo litakuwa ni jambo zuri zaidi.”

Arsenal kwa sasa ipo sokoni kutafuta mshambuliaji na mmoja wa mastaa iliokuwa ikihusishwa nao ni Benjamin Sesko, kutoka RB Leipzig lakini dili linaonekana kufa baada ya kuongeza mkataba mpya.

Mikel Arteta haonyeshi kumwamini sana Gabriel Jesus kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa akiyapata pia kiwango chake kimeshuka katika siku za hivi karibuni.

Neymar mwenyewe aliwahi kuweka wazi siku moja angependa kucheza Ligi Kuu England kutokana na ukubwa wa ligi hiyo na anavutiwa nayo.

“Napenda jinsi timu zao zinavyocheza, nani anajua? siku moja, naweza kuwa hapo, navutiwa sana na Manchester United, Chelsea, Arsenal, Liverpool.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live