Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Newcastle, Man United vita ya Top Four bado mbichi

IMG 3960.jpeg Vita ya top four kati ya Man united na Newcastle bado mbichi

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Newcastle na Manchester United bado vita ya top four ni mbichi baada ya kushinda michezo yao wote siku ya leo katika ligi kuu ya Uingereza na kendelea kufanya vita kupamba moto.

Newcastle wakiwa wametanguliwa katika mchezo wao wa dhidi ya Southampton katika dimba lao la St.James Park walifanikiwa kutoka nyuma na kushinda kwa mabao matatu kwa moja na kufikisha jumla ya alama 65 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Manchester United wao wakiwa kwenye dimba lao la Old Trafford wamefanikiwa kuifunga klabu ya Aston Villa walioko kwenye kiwango bora kabisa, Huku goli pekee liliwapa alama tatu mashetani wekundu likiwekwa kimiani na kiungo Bruno Fernandes na kufanikiwa kufikisha alama 63.

Manchester United na Newcastle bado zinakimbizana na kuhakikisha wote wanamaliza ndani ya nafasi nne za juu lakini kila mmoja akitaka kumaliza juu ya mwenzake, Magpes mpaka sasa wana alama 65 wakiwa wamecheza michezo 33 huku Man United wakiwa wamecheza michezo 32 wakiwa na alama 63.

Newcastle mpaka sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na msimu bora kabisa, Huku Manchester United wakimata nafasi nne kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiachwa kwa alama mbili lakini wakiwa na faida ya mchezo mmoja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: