Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

New Castle yaonja ladha ya ushindi EPL

New Castle United Epl Wilson (kulia) akipachika goli la ushindi kwa Newcastle United dakika ya 40.

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kulikua na upepo mbaya unaopepea ndani ya Klabu ya Newcastle United, hatimaye wamepata ushindi kwenye EPL.

Newcastle United wamekuwa na msimu mgumu kwenye EPL mpaka sasa. Matokeo mabovu yalimuondoa Steve Bruce na benchi lake la ufundi. Ujio wa Eddie Howe ukaleta matumaini mapya kwa mashabiki na uongozi mpya wa klabu. Bado, matokeo yaliendelea kuwa yale yale.

Wikiendi hii, The Magpies walikuwa St James’ Park kuchuana na Burnley. Timu zote zipo kwenye nafasi za kushuka daraja msimu huu, hali ni mbaya zaidi kwa Newcastle ambao wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani.

Kwa mara ya kwanza baada ya michezo 15 ya Ligi Kuu soka nchini Uingereza, Callum Wilson anapachika goli lake la 6 na goli pekee linalowapa ushindi wa kwanza Newcastle United.

Kinachonogesha msimu huu ni kwamba, timu tatu za chini, zote zina pointi 10 mpaka sasa. Mambo yanazidi kunoga!!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live