Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

New Castle United yauzwa kwa waarabu

Pjimage (33) Prince Mohammed bin Salman

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusubiri kwa takribani miezi 18, Klabu ya New Castle United inayoshiriki Ligi Kuu England, imeuzwa rasmi jioni ya Oktoba 7, mara baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa takribani masaa nane.

Mchakato wa safari hii kujadili kuuzwa kwa klabu ya New Castle umeibuka siku chache baada ya klabu hiyo kupoteza mchezo wake dhidi ya klabu ya Wolverhampton wonderers katika mchezo wa Ligi kuu England.

Siku ya Jana mmiliki wa New Castle United Mike Ashley alinukuliwa akisema yuko tayari kuiuza klabu ya New Castle.

New Castle United imeuzwa kwa kiasi cha Pauni milioni 300, sawa na dola za Kimarekani milioni 375 (ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 864,171,159,750).

Wamiliki wapya wa Klabu hiyo ni pamoja na Saudi Arabia Public Investment Fund, Mfuko wa Jamii wa Uwekezaji ambao unasimamiwa na kuongozwa na Mwana mfalme wa Saudia Prince Mohammed bin Salman na wanamiliki hisa kwa 80% ndani ya Klabu ya New Castle.

Hatua hii ni ushindi mkubwa kwa mashabiki wa New Castle ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakichukizwa na uwepo wa mmiliki anaeonmdoka mike Ashley, kutokana na kushindwa kumudu mahitaji ya klabu kwa muda mrefu, kushindwa kufanya usajili wa majina makubwa.

Lakini pia kuna waliochukizwa kwa kuona wamiliki wapya wamepewa sehemu kubwa sana ya klabu.

Vile vile Ligi Kuu ya England imetoa tamko rasmi la mchakato wa kuuzwa kwa klabu ya New Castle kwenda kwa wenyeji hao kutoka Saudi Arabia.

Wamiliki hao wapya wameshaweka mezani ajenda yao kuu, ambayo ni kumuondosha kocha anaekinoa kikosi hicho kwa sasa Kocha Steve Bruce na Antonio Conte, Steven Gerrard, Zinedine Zidane ni miongoni mwa makocha wanaopigiwa chapuo kupewa kibarua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live