Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neville: Kufungwa kizembe itawakosti Arsenal

Arsenal Computer Neville: Kufungwa kizembe itawakosti Arsenal

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

GARY Neville amewaonya Arsenal itakuwa ngumu kwao kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England kama wataendelea kuwa na beki inayoruhusu mabao kizembe kwenye mechi zilizobaki ili kukamilisha msimu huu.

Arsenal inaonekana kuwa na uwezekano wa kunyakua taji la Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza msimu huu tangu mwaka 2004 kwa kiwango chao bora cha uwanjani, wakiongoza msimamo kwa tofauti ya pointi mbili na mchezo mmoja mkononi.

Chama hilo la Kocha Mikel Arteta liliruhusu mabao 16 katika mechi 19 za kwanza kwenye ligi msimu huu, lakini baada ya hapo wameruhusu wavu wao kuguswa mara 12 katika mechi sita za mwisho walizocheza kwenye michuano yote.

Arsenal ilitokea nyuma mara mbili kuwachapa Aston Villa 4-2 uwanjani Villa Park na ilitokea kuchapwa 3-1 na Manchester City katika mechi zao za ligi za hivi karibuni.

Na hapo, Neville - ambaye kwa sasa ni mchambuzi anawaambia Arsenal: “Kitu kimoja nataka kusema Arsenal wajitazame wameruhusu mabao 12 katika mechi sita za mwisho. Kama unakuwa timu inayoruhusu mabao mengi kizembe usidhani kila siku utakuwa na uwezo wa kufunga na hapo utajiweka kwenye wakati mgumu wa kushinda ubingwa.

“Wanapaswa kujitazama kwenye hilo. Wikiendi iliyopita umewarudisha kwenye hali ya kujiamini, lakini wanahitaji kurudi pia kwenye mechi za kucheza bila ya kuruhusu bao - hilo ni muhimu sana. Kuruhusu tu mabao ni kitu wanachopaswa kujichunga nacho sana kwa sababu kitawaweka kwenye ugumu mkubwa.”

Arsenal imepata mzuka wa kubeba ubingwa baada ya kuwachapa Aston Villa baada ya kutokea kupoteza kwa Everton na Man City na iliangusha pointi kwa kutoka sare na Brentford katika mechi zao tatu za mwisho kabla ya kushinda Villa Park.

Chanzo: Mwanaspoti