Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neville Amkingia Kifua Tuchel

Skysports Thomas Tuchel Chelsea 5548914 Neville Amkingia Kifua Tuchel

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKONGWE wa Manchester United, Gary Neville atachukia kuona wanasema Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel yupo kwenye presha japo kwa sasa ana wasiwasi na timu yake.

Chelsea juzi ilipunguzwa kasi ya kuwania ubingwa msimu huu, baada ya kulazimishwa suluhu na Wolves. Kabla ya mchezo huo, waliomba mechi yao isogezwe mbele kutokana na wachezaji wengi kupata maambukizi ila ombi lao lilikataliwa.

Tuchel alilazimika kutumia kikosi dhaifu na hii ilimfanya kushindwa kushinda kwa mara tatu katika mechi zake nne zilizopita.

Chelsea kwa sasa imepitwa kwa pointi sita ndani vinara wa ligi hiyo ambao ni Man City wakiwa na pointi Gary alisema Tuchel hatakiwa kuwa na presha:

“Nadhani bado ana kitu ndani ya benki. Najua klabu yake huwa inafanya mambo yake kitofauti. Lakini nitachukia kusema eti Tuchel yuko kwenye presha hapana zaidi anatakiwa kufanya mabadiliko na hilo sio tatizo kwa upande wake.

“Ila nafikiri unaweza kuwa na wasiwasi kidogo hasa pale mawazo yenu ni kuomba mechi isimamishwe halafu mkaambiwa mcheze inaweza kuwavuruga, ajipange kubadili mambo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live