Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neves amwaga chozi akiwaaga Wolves

Skysports Ruben Neves Football 6197622 Ruben Neves

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ruben Neves alimwaga machozi hadharani kwenye video yake maalumu ya kuwaaga mashabiki wa Wolves baada ya kukamilisha uhamisho wake Saudi Arabia.

Kiungo huyo wa kati wa Ureno, 26, amekubali pesa za Saudi Arabia na amejiunga na Al-Hilal baada ya timu hiyo kutoa Pauni 47 milioni.

Hadi Neves anaondoka Wolves alibakiza mkataba wa mwaka mmoja hata hivyo aligoma kuongeza mwingne na akafanya uwamuzi wa kuondoka.

Nahodha huyo wa zamani wa Wolves alirekodi ujumbe wa video akiwashukuru na kuwaaga mashabiki kupitia akaunti yake ya Twitter.

Neves alipitia baadhi ya takwimu zake na mchango wake ndani ya miaka sita aliyokipiga Wolves pamoja na mabao yake machache ya kuvutia na matukio ya mechi za kimataifa.

Lakini baada ya kuwataja wachezaji wenzake lakini katikati ya video wakati anazungumza alishindwa kuzuia hisia zake akaanza kumwaga machozi.

Neves aliwaambia mashabiki: "Siwezi kuwashukuru vya kutosha mlinikaribisha kwa upendo mkubwa, Siwezi kuwashukuru vya kutosha kwa wema mlionitendea, nitaendelea kuisapoti timu maisha yangu yote, najisikia kama nipo nyumbani na familia yangu haitasahau mema yote,"

Neves alifunga mabao 30 katika mechi 253 alizocheza Wolves na alihusishwa na Barcelona lakini kocha wa timu hiyo Xavi alisema hana mpango wa kumsajili.

Hata hivyo, mashabiki wengi hawakupendezwa na uwamuzi wa kiungo huyo kwani wanaamini ana uwezo wa kucheza katika timu kubwa sita za Ligi Kuu England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live