Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nenda rudi za makocha Ulaya

767474 Jose Mourinho Troubled Reuters?fit=1280%2C720&ssl=1 Jose Mourinho

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea imeripotiwa kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kocha wao wa zamani Frank Lampard ambaye atachukua mikoba ya Ghraham Potter hadi mwisho wa msimu wakati mabosi wa timu hiyo wanaangalia kocha wa kudumu.

Lampard ambaye aliwahi kuifundisha timu hii kuanzia mwaka 2019 hadi 2021 kabla ya kufukuzwa kutokana na matokeo mabaya.

Kurejea kwake kwenye kikosi hiki kunamfanya aingie kwenye orodha ya makocha ambao walifukuzwa kisha wakarejea kuzifundisha timu husika kwa wakati mwingine na baadhi yao walizipa mafaniko na wengine walifeli tena. Hawa hapa makocha saba ambao walifukuzwa kisha wakaajiria tena.

Jose Mourinho

Baada ya kuushangaza ulimwengu mwaka 2004 kwa kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na FC Porto, alipata shavu la kujiunga na Chelsea ambayo kwa wakati huo ilikuwa chini ya bilionea Roman Abramovich.

Akaiwezesha timu hiyo kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu England mfululizo, pia taji moja la FC na Carabao Cup mara mbili.

Aliondoka kwenye timu hiyo mwaka 2007 baada ya kuanza msimu vibaya. Jose alizunguka kisha akarejea Chelsea mwaka 2013 ambapo aliisaidia tena kushinda taji la Ligi Kuu England kabla ya kufukuzwa tena mwaka 2015 kutokana na kuanza vibaya kwa timu hiyo ambayo ilipoteza mechi tisa kati ya 16 za mwanzoni mwa msimu.

Louis van Gaal

Mbali ya klabu kocha huyu wa zamani wa Manchester United ameifundisha timu ya taifa ya Uholanzi katika nyakati tatu tofauti tofauti akienda na kurudi. Kwenye upande wa timu aliwahi kuifundisha Barcelona kuanzia mwaka 1997 hadi 2000 kisha akarudi tena mwaka 2002 hadi 2003.

Kwa mara yake ya kwanza alishinda mataji mawili ya LaLiga twice, Copa del Rey moja na Uefa Super Cup lakini raundi yake yapili kwenye timu hiyo ilidumu kwa miezi saba tu kabla ya yeye mwenyewe kuamua kuachia ngazi akiiacha timu hiyo kwenye nafasi ya 12.

Massimiliano Allegri

Alianza kazi Juventus Julai 16, 2014 hadi Juni, 2019 na katika kipindi chote hicho aliiwezesha timu hii kuchukua mataji matano ya Ligi Kuu nchini Italia na akaifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili ambazo zote alipoteza.

Aliondoka akiwa kocha aliyekuwa na wastani mkubwa wa alama kwa kipindi chote kuwahi kutokea katika historia ya timu hiyo.

Aliajiriwa Andrea Pirlo kama mbadala wake lakini maji yalionekana kumshinda na miaka miwili baadae alifukuzwa kisha Allegri akarudishwa tena ambapo anahudumu hadi sasa ingawa mambo yanaonekana kuwa mabaya kwa sababu timu hiyo inapitia wakati mgumu wa kiuchumi.

Harry Redknapp

Alikuwa kocha wa Portsmouth kuanzia mwaka 2002 hadi 2004 na kabla ya hapo alikuwa akihudumu kama mkurugenzi wa masuala ya michezo.

Alipoondoka kwenye viunga hivyo alitua Southampton ambako alikaa kwa mwa mmoja tu na akaachana nao Desemba 03 kisha Disemba 08 akatangazwa kuwa kocha wa Portsmouth.

Kuanzia mwaka 2002 hadi 2004 akiwa na Portsmouth kocha huyu aliiwezesha timu hii kupanda Ligi Kuu England kisha baada ya kuondoka na kurejea tena katika msimu wa kwanza aliiwezesha kumaliza nafasi ya nane kwenye ligiki kisha msimu uliofuatia akaiwezesha kuchukua taji la FA na baada ya hapo akapata shavu Tottenham Oktoba 2008.

Zinedine Zidane

Mbali ya kuwa na Carlo Ancelotti ambaye aliwahi kuifundisha Real Madrid kabla ya kuondoka na kurudi tena akiendelea kuiongoza hadi sasa, moja kati ya makocha wanaokumbukwa na mashabiki wa Madrid ni mwamba huyu kutoka Ufaransa.

Zidane aliifundisha timu hii kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 ambapo aliiwezesha kushinda taji la Ligi ya Mabingwa mara tatu kabka ya kuondoa na mwishoni mwa mwaka 2018 na kujiunga nao tena miezi 10 baadae mwaka 2019 ambapo alifanikiwa kuchukua taji la La Liga kisha akaondoka mwisho wa msimu wa 2020/21.

Kevin Keegan

Awali Keegan aliwahi kuifundisha Newcastle kuanzia mwaka 1992 hadi 1997, wakati anachukua mikoba ya kuinoa aliikuta ikiwa mkiani kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza kwa wakati huo.

Akaiwezesha kupanda Ligi Kuu kisha akaiongoza kuwa timu tishio kwenye mbio za ubingwa kwa msimu wa 1995-1996 kabla ya kushindwa na kombe kuchukuliwa na Man United.

Mwaka uliofuatia aliamua kujiuzulu mwenye, lakini mwaka 2008 akaitwa tena kuiongoza timu hiyo lakini wakati huu mambo yalikuwa mabaya na akaingia kwenye mzozo na mmiliki wa timu kwa wakati huo Mike Ashley hali iliyosababisha afukuzwe.

Chanzo: Mwanaspoti