Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nenda Mashariki, nenda Magharibi, Bacca ni beki Bora!

Bacca 8028460 Go East, go West, Bacca is the best

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangzaji na mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Clouds Media, Mkazuzu amemmwagia sifa beki wa kati wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Ibrahim Hamad Bacca akisema kuwa mchezaji huyo ni beki bora.

Mkazuzu amesema hayo kufuatia kiwango bora ambacho Bacca ameendelea kukionyesha kwa siku za hivi karibuni akiwa na Stars pamoja na Klabu yake ya Yanga husuani mchezo wa AFCON dhidi ya Morocco licha ya Tanzania kufungwa bao 3-0.

"Go East, go west, Bacca is the best. Sio story tena kuwa Ibrahim Bacca ni moja kati ya walinzi bora sana kwasasa Tanzania ameonyesa ubora akiwa na klabu lakini hata kwenye national team bado anafanya vizuri.

"Ukiangalia performance ya mchezaji mmoja mmoja Bacca alikuwa imara sana, alicheza mipira ya juu, alicheza mipira ya chini kwa usahihi anazuia vizuri, kuhusu sliding tackle kapiga nyingi tena kwa usahihi.

"Namna ambavyo anatumia nguvu na maarifa kwa dakika zote 90 akiwa uwanjani simply unaelewa kuwa ni beki mzuri.

"Ukiangalia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Morocco ni mchezaji mmoja tu ambaye anacheza ligi ya ndani tena anacheza Misri lakini waliobaki wote wanacheza Ulaya so utimamu wao wa mwili ni tofauti na wachezaji wetu wengi ila Bacca bado aliendelea kuwapa shida washambuliaji.

"NB: Simply Ibrahim Bacca is the best defender," amesema Mkazuzu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live