Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nelson Okwa atamba Ihefu

Okwa Ihefu Nelson Okwa

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Ihefu, Nelson Okwa amesema kikubwa kwake ni kupata nafasi ya kucheza kwenye mechi zilizosalia ili kuhakikisha anaonyesha kiwango cha kusaidia timu yake.

Okwa anacheza kwa mkopo Ihefu, akitokea Simba iliyomsajili kutoka Rivers United, lakini hakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Wanamsimbazi, hivyo akaona aende timu anayoweza kucheza.

Baada ya kutua Ihefu, Okwa amefunga bao moja dhidi ya Dodoma, hivyo anatamani kufunga zaidi kadri atakavyopata nafasi ndani ya kikosi hicho.

"Kikubwa kwangu ni nafasi ya kucheza, ili nifanye kitu kwenye mechi zilizosalia kumaliza msimu huu ambao sikuuanza vizuri," alisema.

Alikiri Ihefu ina wachezaji wazuri na wazoefu ambao wanaibua ushindani unaompa chachu ya kuendelea kupambana zaidi kwa ajili ya kumalizia msimu akiwa kwenye kiwango kikubwa.

"Ni kiu ya kila mchezaji kufanya vizuri, kwa sababu soka ni kazi yake, hivyo unapokuwepo ushindani inakuwa sababu ya kuongeza umakini na kupambana kuhakikisha uwepo wangu unakuwa msaada kwenye timu," alisema.

Kocha wa timu hiyo Zuber Katwila alisema "Wachezaji walioingia dirisha dogo wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho ,wanasaidiana na waliopo kuiondoa timu kwenye hatari ya kushuka daraja."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live