Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Neema kwa wadhamini timu za Taifa

Jezi Stars Neema kwa wadhamini timu za Taifa

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Serikali imeahidi kuandaa mazingira bora wa wafanyabiashara na wawekezaji ambao watajitokeza kuzipa udhamini timu za taifa za soka na michezo mingine ili kuzisaidia kukabiliana na changamoto ya kiuchumi pindi zinaposhiriki mashindano mbalimbali.

Akizungumza katika uzinduzi wa jezi mpya za timu za taifa za soka za Tanzania jana, katibu mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa mchango wa wafanyabishara na wawekezaji katika sekta ya michezo una maana kubwa hivyo serikali itawalinda.

'Linapokuja suala la timu ya taifa, hakuna namna ambayo serikali inaweza kujiweka pembeni. Moja kati ya mambo ambayo nitayasimamia ni kutafuta udhamini kwa timu za taifa. Kama unafanya biashara unatengeneza faida Tanzania, Watanzania wanataka furaha. Haipendezi kuona timu za tanzania zinapata changamoto ya kiuchumi na wafanyabiashara na wawekezaji wapo.

"Tutatengeneza uwanja mzuri mje mdhamini timu zetu. Timu zetu zisiwe na 'stress' ya uchumi ziwe na 'stress' ya kufanya vizuri. Hatuwezi kushindwa, tutazungumza namna gani na tutawaandalia tukio kubwa na tutakuwa na kiongozi mkubwa wa kutambua mchango wenu kwa timu za taifa. Wale watakaojitokeza kudhamini timu za taifa, tutawapa jukwaa zuri ambalo mtafurahi," amesema Msigwa.

Chanzo: Mwanaspoti