Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro mgeni rasmi Simba vs Al Ahly

Ndumbaro Pichaa  Data Ndumbaro mgeni rasmi Simba vs Al Ahly

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this AuthorBy Thomas Ng'ituMore by this Author WAZIRI wa Mali Asili na Utalii, Dr Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Jumanne ya wiki ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Simba inashuka dimbani huku ikiwa na mtaji wa pointi tatu mkononi baada ya mchezo wao wa kwanza ugenini kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya As Vita 1-0.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Ijumaa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Haji Manara amesema mgeni rasmi wao ni Ndumbaro.

"Tunaitangaza nchi na Visit Tanzania, tumewaletea na Waziri mwenyewe", amesema Manara

Manara ametamba kwa kusema kuwa, "Simba ndio tunaiwakilisha Afrika Mashariki kwa kuitangaza, tunatangaza nchi pamoja na ukanda wote hakuna timu yoyote iliyopo katika hatua hii."

Simba hivi karibuni ilianza kuitangaza nchi kwenye michuano hiyo baada ya kuingia ubia na wizara hiyo kwa kuvaa jezi zilizoandikwa Visit Tanzania.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz