Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro ayajenga na FIFA, CAF

Fduyuw Ndumbaro ayajenga na FIFA, CAF

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro leo Oktoba 18 amekutana na vigogo wawili wa FIFA na CAF na kufanya mazungumzo nao hapa Dar es Salaam.

Viongozi hao wawili ni Katibu Mkuu wa CAF, Veron Mosengo-Omba na Mwakilishi wa Fifa katika kanda ya Cecafa, Andrea Silva.

Viongozi hao ni miongoni mwa vigogo wa FIFA na CAF waliopo katika msafara wa watu zaidi ya 400 waliokuja nchini kushuhudia mechi ya uzinduzi wa mashindano ya AFL baina ya Simba na Al Ahly, keshokutwa Ijumaa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika kikao hicho, Waziri Ndumbaro na vigogo hao wamejadili maendeleo ya mchezo wa soka nchini ambayo yameonekana kukua kwa kasi kutokana na kufanya vizuri kwa timu za taifa za Tanzania kwa wanawake na wanaume pamoja na zile za klabu kwenye mashindano ya kimataifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, Rais wa TFF, Wallace Karia na makamu wake Athuman Nyamlani, Kaimu Mkurugenzi wa michezo, Ally Mayay, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Neema Msitha na viongozi wengine wa serikali na TFF.

Chanzo: Mwanaspoti