Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro, Nnauye wazindua Wi-Fi ya bure kwa Mkapa

WIFI Mkapa Ndumbaro, Nnauye wazindua Wi-Fi ya bure kwa Mkapa

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

MUDA mchache kabla ya mechi ya Derby inayowakutanisha Simba na Yanga, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano, Nape Nnauye wamezindua intanenti ya bure yaani (Wi-Fi) itakayowarahisishia watu mawasiliano ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umefanyika kupitia mtandao wa simu wa TTCL na intanenti hiyo itaanza kutumika kuanzia leo Novemba 5 na kuendelea.

Mbali na viongozi hao pia alikuwepo Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerson Msigwa.

Chanzo: Mwanaspoti