Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro: Michezo ni biashara sio burudani

Ncytd Ndumbaro: Michezo ni biashara sio burudani

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro amesema kuwa kwasasa Tanzania inatazama michezo kama nyanja mojawapo ya uchumi kwa nchi hivyo inaipa kipaumbele kikubwa.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo katika hafla ya kuzichangia timu za taifa inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Ndumbaro amesema kuwa zama za kutazama michezo kama kitu cha kutoa furaha tu zimeshapitwa na wakati na sasa sekta hiyo ina umuhimu na faida kubwa kiuchumi.

"Sisi tunasema kuanzia sasa ni Wizara ya Biashara. Ni Wizara ya Ajira. Tunatumia michezo, sanaa na utamaduni kama biashara na kama ajira. Ningependa Watanzania wote wajue kwamba kuanzia sasa sisi tunaangalia biashara.

"Tuna mashindano ya timu tano. Shughuli ya timu hizo ni shughuli ya Watanzania. Tuna wadau mbalimbali ambao wako hapa. Kazi hii bado inaendelea.

"Kamati hii ni endelevu. Leo ni uzinduzi wa Harambee lakini tutaendelea nayo kwa mwaka mzima. Tutakuwa na matukio manne kwa mwaka," alisema Ndumbaro.

Chanzo: Mwanaspoti