Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndumbaro: Kuingia kwa Mkapa ja Jezi ya Ahly, Mamelodi uwe na Passport

Gfdtd Ndumbaro: Kuingia kwa Mkapa ja Jezi ya Ahly, Mamelodi uwe na Passport

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea michezo ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika waziri wa utamaduni, sanaa na michezo Mh. Damas Ndumbaro amewasisitiza watanzania kuwa wazalendo katika kuzisapoti timu za Simba na Yanga katika michezo Yao.

Waziri Ndumbaro amesema atasikitishwa endapo ataona watanzania wamevaa jezi za Al Ahly katika mechi ya Simba au jezi ya Mamelod Sundowns katika mchezo wa Yanga huku akisema watu hao hawatoruhusiwa kuingia uwanjani, au wataingia kwa kuonesha Passport zinazoonesha sio Raia wa Tanzania.

“Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo ukifanya fujo Polisi watakuchukua ukapumzike kidogo utatoka baada ya mechi” - Damas Ndumbaro, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo.

View this post on Instagram

A post shared by Shaffih Dauda (@shaffihdauda_)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live