PAPE Malickou Ndoye nyota wa Azam FC ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kubaki ndani ya timu hiyo.
Nyota huyo raia wa Senegal amekuwa na kazi kubwa katika timu hiyo ambayo imekamilisha ligi ikiwa nafasi ya tatu.
Taarifa rasmi kutoka ndani ya Azam FC imeeleza kuwa nyota huyo ambaye ni beki kitasa bado yupo ndani ya kikosi hicho.
“Malickou Ndoye ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu yetu hadi mwaka 2025. Ndoye, ambaye ameungana na kocha wake wa zamani, Youssou_Dabo,” imeeleza taarifa hiyo.
Anaungana na kocha wake wa zamani Youssouph Dabo ambaye naye ni raia wa Senegal atakayeinoa timu hiyo kwa msimu 2023/24.
Azam FC inafanya maboresho ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo kwa msimu wa 2022/23 mabingwa ni Yanga.