Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoto za Miraji Athuman zakatishwa kikatili Simba

99319 Miraj+pic Ndoto za Miraji Athuman zakatishwa kikatili Simba

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

WINGA wa Simba, Miraji Athuman ni kama amejikatia tamaa ya kutimiza ndoto yake ndani ya klabu hiyo badala yake ameamua kutupia mpira kwa Meddie Kagere, anayeona anafanya alichokuwa anakiwazia.

Athuman ambaye aling’ara chini ya kocha Patrick Aussems amekaa nje takribani miezi miwili hivyo anatakiwa kufanya mazoezi ya kuwa fiti ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.

“Moto wangu wa kuzifumania nyavu umepoa, majeraha yalinichanganya kiasi kwamba naona sitaweza kutimiza malengo ambayo nilijiwekea kwenye msimu huu kwa sababu sijawa fiti bado.

“Nimeshaanza kufanya mazoezi ya kusaka kuwa fiti, napiga mahesabu mpaka niwe sawa zitakuwa zimebakia mechi sita halafu tayari kuna wale ambao wamejihakikishia namba ndani ya kikosi cha kwanza, hilo ndilo linaloniumiza kichwa na kuamua kukubali kipindi ninachokipitia,” alisema.

Mchezaji pekee ambaye mpaka sasa anaona njia ni nyeupe kukichukua kiatu cha dhahabu amemtaja ni Kagere ambaye ana mabao 19 na ana bidii ya kusaka mabao zaidi.

Naye Salim Aiyee wa KMC ambaye msimu uliopita alitupia mabao 19, msimu huu kafunga bao moja tu na amebainishia kuumizwa na majeraha.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz