Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndombele achomoa kujiunga na Everton

Ndombele T Tanguy Ndombele

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa kifaransa ambaye anaichezea klabu ya Tottenham Tanguy Ndombele amekataa uwezekano wa yeye kuweza kuhamia klabu ya Everton kipindi hiki cha usajili.

Ndombele licha ya kuigharimu pesa nyingi klabu ya Tottenham, lakini amekuwa mchezaji wa akiba kwenye timu hiyo yenye maskani jijini London tokea Antonio Conte achukue mikoba ya kuinoa klabu hiyo, na ilionekana kuwa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuhama kwenye klabu hiyo kipindi hichi huku Everton wakiwa na nafasi kubwa.

Klabu ya everton kwa sasa inahangaika kutafuta kocha mpya, huku pia wakihataji kiungo wa kati ambaye ataweza saidia safu ya ulinzi nakuweza kunganisha timu kutokea nyuma na kupeleka mashambulizi mbele.

Inaoneka kuwa ameikataao ofa ya Everton ili aweze kujiunga na kocha wake wa zamani Mauricio Pottechino kwenye klabu ya PSG, ambayo nayo imeonesha kuvutiwa na huduma ya kiungo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live