West Ham United imethibitisha Kocha David Moyes ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu, huku kibarua cha kuinoa timu hiyo kikikabidhiwa kwa Mhispaniola, Julen Lopetegui.
Kocha wa zamani wa Wolves, Lopetegui ameripotiwa kufikia makubaliano ya kuinoa West Ham na kugomea ofa ya kwenda kupiga kazi Bayern Munich.
Moyes aliomba radhi baada ya West Ham kuchapwa mabao 5-0 na Chelsea, Jumapili iliyopita, ikiwa ni pigo kubwa kwa timu hiyo katika harakati zao za kufuzu michuano ya Ulaya.
Na taarifa iliyotoka saa 24 baadaye, taarifa ya mwenyekiti mwenza wa klabu hiyo, David Sullivan alisema: “Kwa niamba ya watu wa West Ham United, ningependa kumshukuru David kwa mchango wake aliyotoa kwenye klabu hiyo kwa muda wake aliokuwa kocha.
David amehusika kwenye mafanikio makubwa tuliyopata kwenye historia yetu, amefanya kazi kubwa na kwa kujitolea. Tunamshukuru kwa alichokifanya na tunamtakia mafanikio mengine kwenye maisha yake mengine.
Kwa kusema hilo, tunaomba mashabiki wote tumemfanyia jambo zuri la kumuaga David kwenye mechi yetu ya mwisho ya nyumbani dhidi ya Luton Town, Jumamosi.” Wakati West Ham ikiachana na Moyes, shughuli kubwa kwao ni kupata huduma bora kutoka kwa mastaa wao, Jarrod Bowen, Mohamed Kudus na Lucas Paqueta, ambao walionyesha ubora mkubwa chini yake.A